Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ambae pia ni Mkuu wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mwanza, SSP: Benjamini Kuzaga amewataka askari polisi Wilayani Ukerewe kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya uhalifu ziwani, kwa kuhamasisha wananchi
kushirikiana na Polisi katika kudhibiti uhalifu mdogomdogo ziwani, mfano uvuvi
haramu japo kwa kiasi kikubwa hali kwa sasa ni shwari, lakini tunataka hali iwe
shwari zaidi ili wavuvi wafanye shughuli za uvuvi bila hofu yeyote.
“Amesema tunawapongeza
askari wetu, vyombo vingine vya ulinzi na usalama na wananchi kwa kazi nzuri
wanayoifanya, kwa kuwa hali ya usalama ziwani kwa sasa shwari, hivyo ongozeni
nguvu katika baadhi ya maeneo yenye uhalifu mdogomdogo ambao umekuwa kero kwa
wananchi, mfano ubakaji na utengenezaji wa pombe ya gongo”, alisema SSP:
Benjamini Kuzaga.
Amesisitiza askari
waenda maeneo mbalimbali visiwani hapo kutoa elimu ya Polisi Jamii na
uanzishaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi. Alisema maeneo yote pakiwepo na
vikundi vya ulinzi shirikishi itasaidia kutokomeza uhalifu maana jamii
inawafahamu wahalifu, hivyo hapatakuwepo na makosa ya ubakaji, wizi wa mifugo
wala utengenezaji wa Pombe ya moshi.
Hata hivyo aliwataka
askari kuepuka rushwa kwani sasa sheria inasema kushawishi tu rushwa, ni kosa
kisheria na kwa yeyote atakayebainika anashawishi rushwa hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake. Hivyo aliwataka askari kufanya kazi kwa uweledi huku
wakizingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi.
Kwa upande wake Mkuu
wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Mrakibu wa Polisi, SP: Egnatus Kapira alisema kwa
sasa askari wanayo ari, ujasiri na nguvu ya kufanya kazi hivyo wataendelea
kushirikiana vizuri na wananchi kuhakikisha hali inazidi kuwa shwari. Pia
aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wadau mbalimbali wa ulinzi na usalama
wa Wilayani hapo.