Monday, 19 March 2018

RPC Mwanza awataka Askari Kwimba Kuimarisha Ulinzi shirikishi


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa Polisi, DCP: Ahmed Msangi amewataka askari Polisi Wilaya ya Kwimba kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi vilivyopo na kuanzishi vikundi vingine katika baadhi ya maeneo ambayo hayana, kisha kuwapatia elimu ya Polisi Jamii itakayosaidia kutokomeza uhalifu mdogomdogo unaojitokeza katika maeneo yao. Hayo ameyasema juzi alipokutana na askari wa Wilaya hiyo wakati alipokuwa kwenye ukaguzi.
                                                                                                                                                                                                           DCP Ahmed Msangi 

                                                                                                Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza 

“Wananchi wapewe elimu ya kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika makazi yao, maeneo yenye maduka ya biashara na katika mitaa na vijiji na vitongoji. Kwa kuwaelekeza juu ya namna ya kufanya doria katika maeneo yao na ukamataji salama usio na madhara kwa mhalifu na mkamataji, kisha wahalifu wakifikishwe katika vituo vya Polisi wakiwa salama ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao” alisema Kamanda Msangi.
“Vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi vikipatiwa elimu ya ukamataji salama, itasaidia kuepusha mauaji yanayosababishwa na vikundi vya watu wanaojichukulia sheria mkononi kwa kufahamu au kutofahmu kuwa kufanya hivyio ni kosa la jinai” alisema.
Sambamba na hilo Kamanda Msangi aliwataka askari wa Wilaya hiyo kuongeza mikutano ya Polisi jamii katika vitongoji na vijiji ili kufahamu kero za kiuhalifu zinazowasumbua wananchi na mapungufu ya kiutendaji tuliyonayo sisi Polisi. Jambo hilo litatusaidia sisi polisi kufahamu wapi tumekosea na sehemu ipi tuifanyie kazi.
Aidha pia aliwapongeza askari kwa ukakamavu mzuri waliouonesha wakati wa gwaride, hivyo aliwataka waongeze juhudi hizo pia katika sehemu nyingine za kiutendaji. Pia aliwaeleza askari kuwa kazi wanayoifnya ya kudhibiti uhalifu ni nzuri, hivyo pia waongeze juhudi za kuwakamata watu wanaojihusisha na utengenezaji wa pombe za gongo, wapiga ramli chonganishi, wezi na vibaka.
Kwa upande wa Mkuu wa Polisi Polisi Wilaya ya Kwimba Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP: Yahya Mdogo alishukuru Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya, vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi kwa ushirikiano mzuri wanaompati. Vilevile aliahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote aliyopatiwa na Kamanda na mabadiliko yataonekana.

Subscribe to get more videos :