Taasisi
zinazojihusisha na utoaji wa huduma za bima zimetakiwa kutumia mfumo wa wa
kielekitroniki wa TIRA MIS ili kuhepuka usambazaji wa stika bandia
Kauli hiyo
imetolewa na kaim mkuu wa mkoa wa mwanza dk leonald Masale wakati wa uzinduzi
wa mfumo wa kuhakiki stika kwa njia ya kielekitriniki
Masale
amesema kufanya hivyo kutalisaidia taifa kupata mapato lakini pia jamii husika
itanufaika na kuepuka kupewa stika za kughushi
Kwa upande
wake kamishna wa bima nchini dk Baghayo saqware amesema kwamuda mrefu wateja
wamekuwa wakiibiwa kwa kupewa stika za bima zisizostahili.
Aidha taifa
limekuwa kipoteza mapato kutokana na kadhia hiyo na hivyo kwa kutumia mfumo huo
mteja ataweza kuhakiki stika ya kile alichokilipia.