Ni katika ijumaa ya mwisho kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan ambapo CITY FM MWANZA pamoja na LUCKY TV zimewapokea Mashekhe kutoka nchi hizo tatu na kupata fursa ya kushiriki katika kipindi cha Ijumaa njema kinachorushwa kila ijumaa kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa saba mchana.
Jopo Kutoka kenya limeongozwa na shekh Mohamed Kusoma Kutoka mombasa, Burundi jopo lao likiongozwa na Shekh Fadhil Juma Uthman Bombe Imam mkuu wa Masjid Shafii Istiqama Bunyezi Bujumbura, wakati Tanzania jopo likiongozwa na Imam wa Mskiti wa Shamsia Kirumba wilayani Ilemela ,Shekh Sururu Salum Iikiwemo jopo la jumuiya ya ISUWAT MWANZA na SIMIYU chini ya mwenyekiti wake Shekh Ahmed Yussuf.
Katika kipindi hicho, kwa pamoja wamesisitiza jamii kuupokea vyema mwezi mtukufu wa Ramadhan, kuufunga mwezi huo,kufanya ibada,kuwathamini maskini, kutoa sadaka, na kuacha kufanya matendo maovu.
Aidha wageni hao wamepokelewa na uongozi wa city fm pamoja na lucky tv akiwemo mwongozaji wa kipindi cha Ijumaa Njema Muzamilu Yusuph.