Saturday, 27 May 2017

Wakuu G7 kuangazia Afrika na janga la wahamiaji

media
Wahamiaji haramu wakijaribu kuingia Ulaya walikusanyika Tajura kituo cha Tripoli, May 9, 2017.MAHMUD TURKIA / AFP Afrika



Viongozi wa nchi zilizostawi kiuchumi duniani G7 wanataraji kukutana na viongozi wa bara la Afrika baadae kwa mazungumzo juu ya janga la wahamiaji.
Viongozi kutoka Tunisia, Kenya, Ethiopia, Niger na Nigeria watazungumza na wakuu hao katika siku ya pili ya mkutano wa G7 mjini Taormina, Sicily.
Italia ilichagua kuwa mwenyeji wa mkutano huo ili kuvutia umakini kwa Afrika na mamilioni ya wahamiaji ambao wamekuwa wakihatarisha maisha yao kuelekea Ulaya.
Hata hivyo mjadala mkali ambao umeendelea kutawala vikao vya G7 ni kuhusu ugaidi na mabadiliko ya tabia nchi.

Chanzo-Rif swahili

Subscribe to get more videos :