Jamii imetakiwa kuwa
makini na ugonjwa wa homa ya ini ugonjwa ambao umekuwa ukileta madhara
katika jamii .
Hayo yamesemwa na Dr. Edwin Masue ambaye ni daktari
bingwa wa magonjwa ya ini alipokuwa akizungumza na city fm juu ya athari ambazo
zinatokana na ugonjwa wa homa ya ini ugonjwa ambao kila kukicha unazidi kuwa ugonjwa
hatari katika ukanda wa jangwa la sahara.
Dkt masue amesema kuwa ugonjwa huo unasababishwa na
vitu mbalimbali kama ulaji wa vitu vyenye sumu lakini pia unaweza kuwapata
watumiaji wa muda mrefu wa pombe kali .
Aidha ameitaka jamii kuwa makini na kujiepusha na vitu ambavyo vinaweza
kupelekea kupata ugonjwa wa homa ya ini
kwani wengi wao wanapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo watu ambao ni nguvu
kazi ya taifa