Serikali
inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kunusuru maisha na mali za wananchi
kutokana na kuwepo kwa ongezeko la wanyama wakali na waharibifu hapa nchini.
Hayo
yamesemwa leo bungeni jijini Dodoma wakati wa maswali na majibu na Mh.Waziri wa
maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe alipokuwa akijibu swali la
Mh.Godluck Mringa mbunge wa jimbo la Uranga.
Profesa
Maghembe ameongezea kwa kusema kuwa hatua hizo ni pamoja na kufanya doria za
wanyama wakali na waharibifu ili kudhibiti madhara ya wanyamapori hao kwa
kutumia Askari wa wanyamapori waliopo katika pori la seluhu eneo la
Ironga,kikosi dhidi ya ujangiri pamoja na kutoa elimu juu ya uhifadhi kwa jamii kuhusu kujikinga na wanyama hao
wakali wakiwemo tembo na viboko.
Aidha
amesema kuwa wizara imekuwa inafanya majaribio ya kutumia ngede zisizokuwa na
Rubani kwa ajili ya kufukuza tembo pindi wanapovamia makazi na mashamba ya
wananchi.