Mgeni Rasmi, Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongela (wa kwanza kulia) akimkabidhi cheti cha
pongezi Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza Mzee
Enock Masele (wa pili kushoto) kwa mchango wake ndani ya chama hicho.Chama
Kikuu cha Ushirika Nyanza kilitoa vyeti vya pongezi kwa viongozi mbalimbali
wakiwemo Rais Dkt.John Magufuri pamoja
na waasisi wa chama hicho akiwamo Marehem Mark Boman.
Na Mwandishi wetu
LUCKY MEDIA GROUP.
Bodi
ya Mpito ya Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza imemwagiwa sifa Rukuki kwenye
Mkutano Mkuu wa 26 wa chama hicho uliofanyika jana katika ukumbi wa Bomani
(Nyanza) Jijini Mwanza.
Wajumbe
wa mkutano mkuu huo ambao pia ulikuwa na ajenda ya uchaguzi wa viongozi wa Bodi
ya Nyanza, waliipongeza bodi ya mpito chini ya mwenyekiti wake Enock Masele kwa
kazi kubwa ikiwemo kufanikiwa kurejesha mali tisa kati ya 10 za Chama cha
Ushirika Nyanza, zilizodaiwa kuuzwa kinyemela.
Pia
benki ya CRDB kupitia kwa Meneja Biashara Danford Muyango ilieleza utayari wake
wa kuhakikisha chama hicho kinarejea na kuendelea na shughuli zake kama kawaida
na kuondokana na hatihati ya kufirisika kama ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye alikuwa mgeni Rasmi aliwaasa wanachama kuwa
makini na viongozi wao kwani wao ndo watakaoifanikisha kuirejesha heshima ya
Nyanza kama ilivyokuwa awali katika miaka ya 70.
Mkutano
huo pia uliridhia vyama vya msingi kutoka Geita na Simiyu kujitenga na Chama
Kikuu cha Ushirika Nyanza ambacho sasa kitakuwa na Vyama vya Msingi kutoka mkoa
wa Mwanza pekee. Mikoa iliyojitenga inakwenda kuunda Chama Kikuu cha Ushirika
katika mkoa husika hii ikiwa ni kwa mjibu wa sheria kama alivyobainisha Kaimu
Naibu Mrajisi-Udhibiti Collins Nyakunga kwenye mkutano huo.