daktari bingwa wa Macho katika hospital ya rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.
Na Mwandishi wetu
LUCKY MEDIA GROUP
Hospital ya Rufaa ya
Bugando Mkoani Mwanza inaendesha zoezi la uchunguzi wa Macho kwa watoto wadogo
ambao wana matatizo ya macho ikiwa ni sehemu kuwasaidia wanajamii katika mkoa
huo.
Daktari wa macho katika
hospital ya Bugando Dakta Evarista Mgaya
ameitaka jamii kujenga tabia ya kuhudhuria katika vituo vya afya vinavvyotoa
huduma ya macho ili kuweza kupima afya ya macho.
ili kuepukana
na upofu unaoweza kujitokeza ambapo amesema kuwa zoezi hilo linaenda
sambamba na kupima na kuwafanyia upasuaji wale watakaobainika kuwa na uhitaji
wa huduma hiyo.
Amesema kuwa kitendo cha watu kuchelewa kupata huduma ya
matibabu ya macho inapelekea tatizo hilo kuwa kubwa zaidi ambapo wapo watoto
ambao pia wamezaliwa bila kuona.
Kwa upande wake Mratibu
wa Macho toka Hospital ya Rufaa ya KCMC Mkoani Kilimanjaro Bw Henry Mareawe
amesema kuwa watoto watakaobainika kuwa na uhitaji watapata huduma ya upasuaji
na dawa bure