Mwili wa binadamu unafanya mambo mengi ya kibaiolojia ambayo mara nyingi ni vigumu kuyaelewa.
Mwili una mifumo mbalimbali ya ulinzi ambayo inatulinda na hatari
zinazoweza kutudhuru. Mifumo hiyo inatulinda masaa 24 ya siku, Siku zote
7 za wiki, katika mambo yote yanayoweza kuhatarisha maisha yetu.
Yafuatayo ni mambo yanayofanywa na mwili ambayo ni kati ya hiyo mifumo ya ulinzi wa mwili wa binadamu.
1. KUPIGA MIAYO (YAWNING)
Lengo kubwa la kupiga muayo ni kuupoza ubongo baada ya joto kuzidi kwenye ubongo au baada ya ubongo kuchoka kufanya kazi.
Vile vile kama ukiwa umechoka au una njaa husabababisha oxygen kupungua
kwenye damu na kwenye mapafu, hii hupelekea tatizo la kupumua, hivyo
kupiga miayo husaidia kuingiza oxygen ya ziada mwilini ili irudishe
mwili katika hali yake ya kawaida.
2. KUPIGA CHAFYA (SNEEZING)
Mara nyingi tunapiga chafya pale pua zetu zinapokua zimejaa bakteria wa
magonjwa ambao hawahitajiki mwilini, Vumbi pamoja na takataka mbali
mbali zilizoingia kupitia pua.
Hivyo kupiga chafya ni kitenda cha mwili kujisafisha kwa kuyatoa hayo matakataka nje yaliyoingia mwilini.
3. KUJINYOOSHA (STRETCHING)
Kuninyoosha mwili ni kitendo kisicho cha hiari ambacho lengo lake ni
kuuandaa mwili kwa ajili ya kazi mbalimbali za kutumia nguvu
utakazokabiliana nazo kwa siku nzima. Lakini pia kujinyoosha kunaipa
misuli ya mwili mazoezi na kuiweka sawa vilevile kunarudisha mzunguko wa
damu katika hali yake ya kawaida na kumtoa mtu katika uchovu.
4. KWIKWI (HICCUPING)
Najua umewahi kupata kwikwi, na mara nyingi mara baada ya kumaliza kula
chakula. Je umeshawahi kujiuliza ile sauti ya ajabu ya kwikwi
inasababishwa na nini au kwa sabababu gani watu hushikwa na kwikwi?
Hiyo yote husababishwa na DIAPHRAGM (tamka DAYA - FRAM) kiungo
kinachopatikana ndani ya mwili wa binadamu chini kabisa ya kifua baada
ya mapafu(lungs). Kazi kubwa ya diaphragm ni kusaidia katika upumuaji,
(inhale) na (exhale). Pale unapoingiza hewa ndani (inhale) diaphragm
hushuka chini ili kusaidia kuivuta hewa ifike kwenye mapafu. Na unapotoa
hewa nje (exhale) diaphragm hutulia kwa kubakia sehem yake ili
kuwezesha hewa chafu kutoka nje kupitia pua na mdomo.
Sasa basi, kuna wakati diaphragm kubugudhiwa na kuisababisha kushuka
chini kwa kasi sana jambo linalosababisha wewe kuvuta hewa (inhale) kwa
kasi isiyo ya kawaida kupitia koromeo la sauti, hewa ikifika kwenye box
la sauti (larynx), sehem hiyo hujifunga kwa haraka sana ili kuzuia hewa
isipite huko na ndipo KWIKWI hutokea.
Mambo mengine yanayoweza kuibugudhi diaphragm na kuisababisha kufanya
kazi vibaya mpaka kupelekea kwikwi ni kitendo cha kula haraka haraka au
kuvimbewa.
5. KUJIKUNJA KWA NGOZI YA VIDOLE VYA MIKONO BAADA YA KULOWA AU KUKAA MUDA MREFU KWENYE MAJI
Je, umewahi shuhudia jinsi ngozi ya vidole vyako inavyojikunja baada ya
kufua nguo muda mrefu au kushika maji muda mrefu? Unajua ni kwa sababu
gani ngozi hujikunja kama ya mtu aliyezeeka angali yu kijana mara baada
ya kukaa sana kwenye maji?
Watu wengi kabla walizani kwamba kujikunja kwa ngozi hiyo hutokana na
maji kuingia kwenye ngozi na hivyo ngozi hujikunja baada ya kulowa.
Lakini wanasayansi baada ya kufanya utafiti kwa muda merefu juu ya nini
hasa hupelekea ngozi kujikunja? Walisema HAPANA si kwa sababu ya ngozi
kulowana. Na walikuja na majibu haya.
Mwili unapokutana na majimaji mara moja hupeleka taarifa na kutafsiri
kwamba mazingira hayo yana UTELEZI (Slippery) hivyo kutasababisha mikono
kushindwa kushika (Grip) au kukamata vitu kwa urahisi kutokana na
utelezi huo. Hapo mwili huchukua hatua ya haraka kuikunja ngozi ya
mikono yako ili kurahisisha ushikaji wa vitu vinavyoteleza ndani ya maji
pamoja na kutembea kwenye utelezi.
6. VIPELE VIPELE VYA BARIDI KWENYE NGOZI (GOOSEBUMPS)
Kazi kubwa ya vipele hivi ni kupunguza kiasi cha joto la mwili
linalopotea kupitia matundu ya ngozi. Hivyo kwa kufanya hivi humfanya
binadamu kutunza joto la mwili hata katika mazingira ambayo hali yake ya
hewa si rafiki kwa mwili wa mwanadamu au ni yenye baridi sana.
7. MACHOZI (TEARS)
Zaidi ya kuwa majimaji (MUCOUS MEMBRANE ) yanayopatikana kwenye Macho
ambayo kazi zake ni kulilinda jicho dhidi ya kitu chochote kigeni
kinachoingia jichoni (mfano unapokata vitunguu au mdudu anapoingia
jichoni huwa unatoa machozi mengi eeeh!! Pia dhidi ya upepo na moshi) na
pia hutumika kama kilainishi cha jicho pale linapokuwa linazunguka
zunguka (blink).
Vilevile machozi yana kazi ya kupunguza HISIA ZA HUDHUNI zinazozalishwa
mwilini. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu anapokua mwenye msongo wa mawazo
(stress) mwili hutengeneza kitu kipya ili kwenda kubugudhi na kuharibu
maumivu yote ambayo mtu anajisikia. Hivyo machozi yanayozalishwa hapa
huwa na kemikali na yanafahamika kama NATURAL PAINKILLER. Machozi haya
ni tofauti na machozi ya kawaida, lengo lake hasa la kuzalishwa ni kwa
ajili ya kuondoa kabisa maumivu yaliyozalishwa mwilini
Hivyo mpaka hapa tumeona kua kuna machozi ya aina tatu ambayo ni
i. Basal tears (vilainishi)
ii. Reflex tears (mlinzi)
iii. Emotion tears (mtuliza maumivu)
8. KUSHTUKA USINGIZINI (MYOCLONIC JERKS or HYPNIC JERK)
Je! Ushawahi kutokewa na hali hii? umelala halafu ghafla unashtuka
usingizini kwa mguvu nyingi kama umepigwa na shoti ya umeme na akili
inakurudi ghafla huku mapigo ya moyo yakikuenda mbio? Na hali hii
ikakutokea pasipo hata kuota ndoto yoyote?
Basi usiogope au kuwasingizia watu uchawi, hii ni hali ya sayansi ya
mwili.na ni njia moja wapo katika ile mifumo ya mwili kujilinda.
Je, hutokeaje?
Hii ni hali ya ajabu sana isiyofanywa kwa hiari ambayo huwatokea watu
mara tu wamejinyoosha kitandani na kupitiwa na usingizi, mwili
hutetemeshwa na kusukumwa kwa nguvu na mtu hushtuka katika hali kama
vile kapigwa na shoti ya umeme. Hali hii inaweza kupelekea mtu hata
kuanguka kitandani na humwamsha mara moja kutoka usingizini.
Wanasayansi wanatuambia kua, pale tu unapopata usingizi kiwango cha
upumuaji kinashuka ghafla, mapigo ya moyo nayo taratibu yanapungua,
misuli inatulia kwa ku-relax, Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali
hii kama ni DALILI ZA KIFO (brain's misinterpretation of muscle
relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za kuushtua mwili kwa
kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu, hali ambayo humfanya mtu kuamka
kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida.
Hali hii ikimtokea mtu huambatana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo
(rapid heartbeat), kuhema haraka haraka, na wakati mwingine mtu hutokwa
na jasho jingi.
Wakati mwingine mtu huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae
huishia hukuangalia tu huku akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi
kuna tatizo gani?
MWILI WAKO NI ZAIDI YA UNAVYOUJUA. JAMBO LA MSINGI NI KUONDOA HOFU KWANI
MWILI WAKO UNAJUA NINI UFANYE NA WAKATI GANI ILI KUKULINDA USIKU NA
MCHANA KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.
Source: JF