July 15,
2017, timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars ilicheza mechi yake ya kwanza
katika uwanja wa CCM KIRUMBA kwa
wachezazaji wanaocheza ligi za ndani ili kuwania tiketi ya ushiriki wa michuano
ya mataifa ya Afrika CHAN 2018, ambapo
ililazimishwa sale ya gori 1-1 dhidi ya timu ya taifa ya RWANDA.
Mchezaji Dominique Nshuti wa timu ya taifa ya Rwanda aliiandikia bao la
kuongoza timu yake dakika ya 17 kufuatia makosa yaliyofanywa na mchezaji wa Taifa
Stars ambae ni majeruhi Shomari kapombe ambae alitoka na kuingia Boniface maganga
Mchezo
wa vuta nikuvute huku timu zote mbili zikionyesha uwino sawa uwanjani, Taifa
stars walifanikiwa kusawazisha goli na kubadili matokeo dakika ya 34 kupitia
nahodha wake Hamid Mao kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji Mico Juastin kuunawa mpira katika eneo
la hatari na kufanya matokeo kuwa Taifa stars 1-Rwanda 1.
Timu
zote mbili zilifanya mabadiliko ambapo Taifa stars walimtoa mchezaji John Bocco na nafasi yake kuchukuliwa
na Stamil Mbonde na kufanya mchezo
kubadilika japo mabadiliko hayo hayakuzaa matunda.
Hadi
mchezo unamalizika mabao yalikuwa 1-1 ambapo sasa Taifa Stars wanakibarua
kikubwa katika mchezo wa marudiano, mchezo utakaochezwa Kigali- Rwanda tarehe
23 mwezi wa saba 2017 na ili Taifa stars ifuzu kuingia hatua inayofuata
inatakiwa ishinde kuanzia 1-0 au kama ni sale basi iwe sale kuanzia mabao 2-2.