KAMANDA WA POLIS MKOA WA MWANZA AHMED MSANGI |
Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polis mkoani
mwanza kwa kumfanyia ukatil mwanae .
Tukio hilo limetokea
may 25.05.2017 majira ya saa 05:00hrs
alfajiri katika mtaa wa Ndofe wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza, Bw Nuhu James
miaka 50 mkazi wa Ndofe, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumfanyia
ukatili mtoto wake aitwaye wa kiume miaka 14, mwanafunzi wa kidato cha pili shule
ya secondary Igoma kwa kumfunga kamba miguuni na mikononi kisha kumchapa fimbo
sehemu mbalimbali za mwili wake na baadae kumkata na kisu sehemu za makalio,
kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Inasemekana kuwa baada
ya mama wa mtoto kuona ukatili aliofanyiwa mtoto wake na hali yake ya kiafya kuzidi
kubadilika alishindwa kuvumilia ndipo tarehe 28.05.2017 alikwenda kituo cha polisi
kutoa taarifa. Askari walifanya ufuatiliaji wa haraka kuhusiana na taarifa hizo
na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa
aliaamua kumfanyia ukatili wa aina hiyo mtoto
wake baada ya kugundua kwamba mwanae ni mtoro shuleni. Polisi wapo katika
upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa, pindi uchunguzi ukikamalika mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani, majeruhi amepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu na
hali yake inaendelea vizuri.
Kamanda wa polisi mkoa
wa mwanza naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji
na mkoa wa Mwanza hususani wazazi/walezi kuacha tabia ya kuwapa adhabu ya
vipigo watoto pindi wanapokosea bali wanatakiwa wakae na watoto wao kisha
wawaelimishe kuhusu maadili mema na mabaya, ili kuepusha matatizo ya aina kama
hii kwa wazazi, au ajali na vifo vinavyoweza kuzuilika.