Katika hali
isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara wa samaki jijini Mwanza Bw. Maxmiliani
Ngedele mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa
mtaa wa Kanyerere Kata ya Butimba wilayani Nyamagana mkoani Mwanza amemuua
mkewe kwa kumpiga risasi Mgongoni na kutokea tumboni kisha yeye kujiua kwa kujipiga risasi kifuani
.
Tukio hilo limetokea usiku wa Tarehe 25 mwezi
huu majira ya saa tano usiku katika nyumba
yao iliyopo mtaa huo baada ya kutokea sintofahamu kati ya wanandoa hao hali
iliyopelekea mume kuchukua maamuzi magumu ya kumpiga risasi mkewe aitwae Tedy
Patrick miaka 38 na yeye kujiua kwa
kujipiga risasi.
Mtoto wa marehemu hao aitwaye Ester
Maximillian alieleza kuwa, Siku ya tukio baba yake Bw. Maximilian alifika
nyumbani majira ya saa nne usiku akitokea kazini kwake na yeye ndio
alimfungulia mlango na wakasalimiana vizuri lakini wakati mama yake Bi. Tedy
Patrick akifika nyumbani kwake majira ya saa tano usiku na alifunguliwa mlango
na mfanyakazi wao,
Baada ya mfanyakazi kumfungulia mama
mlango alikuja na kunieleza kuwa mama amelewa kweli alipoingia ndani alikuja
hadi chumbani kwetu akiwa naongea maneno ambayo siyo mazuri huku baba akiwa
amekaa kimya na baada ya hapo waliingia chumbani kwao na kujifungia na sisi
tukaingia chumbani kwetu,
Lakini baada ya muda tukasikia milio ya
risasi na kelele za baba akisena nataka kujiua tulipoenda nikamwambia baba
usijiue kwani utatuacha na nani hapo nikasikia mama anamuomba msamaha baba kuwa
amsamehe kwa kile kilichotokea baada ya hapo sisi tukarudi chumbani,
Lakini baada ya muda tulisikia mlio wa
risasi tulipoenda tukakuta mama anavuja damu huku baba akiwa amekufa tayari na
neon la mwisho alilotuambia mama alisema mnikimbize hospital kwani amebaki yeye
tu wa kuwasaidia,
Na tulivyoita majirani wakamkimbiza
hospital kwa ajili ya matibabu lakini na yeye amefariki akiwa hospital
akipatiwa matibabu.
Ester aliendelea kueleza kuwa hajawahi
kuona wazazi wake wakigombana hadi kupigana bali walikuwa wanakaa pamoja wakati
wa jioni na kushauriana mambo mbalimbali ya kimaisha na biashara zao lakini
ugomvi haukuwepo.
Jirani wa marehemu yao aliyejitambulisha
kwa jina la Jani Malegesi alisema siku ya tukio walisikia milio ya risasi
wakadhani mtaa umevamiwa na majambazi wakati wanatafakari nini kinatokea katika
mtaa wao wakasikia mlinzi wa jirani yao huyo akiwaita kuwa wanahitaji wakatoe
msaada na walipofika walikuta damu nyingi zimezagaa katika chumba cha wanadoa
hao huku Maximillian akiwa amekata roho,
Ikanibidi niwatulize wale watoto na
baada ya hapo nilipiga simu polisi na walipo kuja tulimpeleka Tedy Hospital kwa
ajili ya matibabu lakini alfajiri ya kuamkia Tarehe 26 tukapata taarifa kuwa
naye amefariki dunia,
Kweli hatukuwahi kusikia kama wanaugomvi
wa aina yeyote kwani wanamuda mchache sana tangu walipohamia kwenye nyumba yao
hiyo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kanyerere Bw.
William Ngongo alieleza kuwa taarifa alizipata majira ya saa 11 alfajiri jambo
ambalo lilimfanya kufika kwenye tukio na alipofika alikuta mwili wa marehemu
umepelekwa hospital na mama wa familia na naye alikuwa amekufa kwa kweli
tumesikitishwa sana kutokana na familia hii nilikuwa naifahamu vizuri sana,
Bw. William alisema jeshi la polisi
linatakiwa na serikali wanatakiwa kutoa silaha kwa kuangalia mtu ambaye wanampa
silaha za moto ili kupunguza matukio kama hayo yanayojitokeza katika maeneo
mbalimbali hapa nchini hasa kwa kuwahusisha viongozi wa serikali za mitaa ili
waweze kuja watu wanaomiliki silaha katika mitaa yao.
Kamanda wa polis mkoani Mwanza Naibu
kamishina wa polisi Ahmed Msangi amesema kuwa taarifa za awali zinabainisha
kuwa wawali hao walitokea kutoelewana
ndani ya nyumba hiyo ndipo majirani waliposikia milioni ya riasi kisha
kufika na kukuta mwanaume akiwa amelala tayari amepoteza maisha huku mwanamke akiomba msada na
kukimbizwa hospital ambapo amefariki wakati akipewa matibabu
kamanda Msangi amesema kuwa chanzo cha tukio
hilo la wanandoa hao bado halijafahamika kutokana na wote kupoteza maisha lakini uchunguzi bado
unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Hata hivyo Kamanda Msangi amewataka wakazi
wa jiji la Mwanza iwapo wanamatatizo ya kifamilia hususani masuala ya
mali,mahsusiano ni vyema kufika kwa viongozi wao wa mtaa pamoja na viongozi wao
wa dini ili kupata ushauri na kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea
ikiwamo vifo na kuacha watoto katika mazingira magumu ya maisha.
Aidha alisema kutokana na matukio kama
hayo kujitokeza mara kwa mata jeshi la polisi mkoa wa mwanza linajipanga
kutengeneza mfumo mzuri wa kuwamilikisha watu silaha ikiwemo mtu kupimwa akili
ili kupunguza matukio ya aina hiyo.